
Mahindi ni chakula muhimu na ni aina ya nafaka katika mataifa ya Afrika
yaliyomo kusini mwa jangwa la Sahara. Ni chakula cha matumizi ya
nyumbani kwa idadi ya watu inayokadiriwa kuwa asilimia 50. Ni chanzo
muhimu cha madini na kuongeza nguvu mwilini, protini, madini ya chuma
(iron) vitamini na madini mengine asilia.Waafrika hutumia mahindi kwa
njia mbalimbali – (uji, ugali na pombe). Na mahindi ya kuchoma. Kila
sehemu ya mmea wa mahindi ina thamani kiuchumi : punje, majani, shina na
magunzi huweza kutoa kiasi kikubwa cha bidhaa nyinginezo zilizo chakula
na zisizokuwa chakula.
KANUNI YA KWANZA
Panda mapema
Tayarisha shamba mapema kwa zana yoyote iliyo ndani ya uwezo wako (jembe, maksai, trekta).
Kwa wilaya ya Mbozi Panda kuanzia tarehe 15 Novemba hadi kati kati ya mwezi Desemba.