Monday, April 13, 2015

Wafanyabiashara wa vitunguu Singida walia na Waganda, Wakenya


Singida. Wafanyabiashara wa vitunguu katika Soko la Misuna, Singida wameiomba Serikali kuwasaka na kuwakamata wafanyabiashara kutoka Kenya na Uganda wanaonunua zao hilo moja kwa moja kutoka kwa wakulima kwa madai kuwa wanawanyonya wakulima na kuikosesha halmashauri mapato.